Katika kuhakikisha kina mama wilaya ya pangani wanasonga mbele kimaendeleo leo kinamama wa kikundi cha AMANI GROUP cha Pangani Magharibi wameitisha kikao huku lengo la kikao hicho ni kufanya harambee ili kuwasaidia kinamama hao.
Na huku Bi zainabu akiendesha harambee
hiyo, Mbunge wa viti maalum Pangani Saumu Sakala ametoa shilingi laki mbili,Mbunge Jumaa Hamidu Aweso
ametoa laki tatu,mwenyekiti wa kata ya pangani magharibi laki tatu,katibu wa
wafugaji wilaya laki mbili huku viongozi wengine wa vyama wakitoa fedha katika
harambee hiyo.
Pia katika harambee hiyo Mbunge
saumu sakala ameahidi kuwaletea wakinamama wa kikundi cha Amani Group Mwalimu
wa kuwafundisha Ujasiria mali ili kipato cha wakinamama hao kuongezeka .
Na kwaupande wake Mbunge Jumaa
Hamidu Aweso wakati akitoa neno katika harambee hiyo amewataka wakina mama hao
kuandika barua ili kuweza kupa fedha zinazo tokana na mfuko wa jimbo.
kwaupande wake mkuu wa wilaya ya
Pangani Bi Zainabu amewapongeza wakinamama hao kwaku thubutu kuanzisha kikundi
chao kwa lengo la kuwakwamua wakina mama.
Lakini amewataka wakinamama hao
kukisajili kikundi chao halmashauri ili hata wakati wa kutoka asilimia 5 ya
halmashauri na wao wawezekupata fedha kwaajili ya maendeleo ya kikundi hicho.
Hatahivyo Bi Zainabu hakuwacha
kuwashukuru wabunge kwakuacha mda wao na kukubali kuja katika harambee ya
kikundi cha kinamama cha Amani Group cha Pangani Magaribi,na huku akiwaomba kuwa pamoja katika kupeleka
maendeleo ya Pangani mbele.
Hivyo katika harambee hiyo ya kikundi cha kina mama
cha Amani Group mkuu wa wilaya Bi Zainabu ametaja fedha zilizo patikana ni
shililngi Milioni Moja Laki Saba na Elfu Arubaini Kwaajili ya kuwasaidia wakina
mama hao.