Mbunge Saumu Sakala akikagua Jengo la Shule iliyo Jengwa kupitia nguvu za wananchi katika kata ya Sigaya Wilayani Mkinga |
Mbunge Saumu Sakala
amendelea na ziara ya kata kwa kata wilaya kwa wilaya katikawilaya ya mkinga
kata ya sigaya.
Katika ziara hiyo
aliongozana na wenyeviti na diwani wa viti maalum kujua changamoto zinazo wakabili
wanakijiji wa kata ya sigaya iliyoko wilaya ya mkinga.
Mbunge amejionea
changamoto ya wahamiaji haramu kutoka kenya inayo wakabili wakazi wa kata hiyo,ambapo
wahamiaji hao wamekua wakiharibu mazingira kwa kukata miti na kwenda kuuza
kenya.
Wananchi hao pia
wamelalamikia suala la wizi wa mifugo unao fanywa na wahamiaji hao huku
wakisema wahamiaji ni kutoka kabila la waduruma na wakamba ambao baada ya kuiba
mifugo huenda kuuza kenya.
Kunyang’anywa kwa
vitambulisho vya ukazi kwa baadhi ya raia ambao ni WATANZANIA huku mamlaka
husika wilayani mkinga ikidai ni wahamiaji kutoka kenya.
Pia wananchi wa kata ya
sigaya wamelalamikia changamoto ya
kutokamilika kwa shule ya msingi iloiyojengwa kupitia nguvu za
wananchi,vyoo pamoja na kutokamilika kwa nyumba za wauguzi katika kata hiyo .
Suala ambalo Mbunge
Saumu Sakala amehuzunika sana hatua ya
shule iliyojengwa kupitia nguvu za wananchi na serikali kushindwa kuwasidia
wananchi hao kukamilisha shule hiyo.
Lakini kufuatia
changamoto hizo Mh Mbunge Saumu Sakala ameahidi kufuatilia matatizo hayo na
kuwaambia wana kata ya sigaya kuwa atakutana na Waziri wa mambo ya ndani juu ya
kupambana na suala la wahamiaji haramu kutoka kenya.
Pia mbunge saumu sakala
aliendelea na ziara yake katika kata tatu ambazi ni kata ya Boma Ndani ,Mkinga
Mjini,na kumalizia katika kata ya kwale ambapo alikutana na chamgamotom nyingi
ambazo kwanamna moja ama nyingine zinarudisha maendeleo ya wilayaya mkinga.
Miongoni mwa changamoto
hizo ni ubovu wa barabara katika kata ya Boma Ndani ambayo kwa wakati wa mvua
watoto wa shule huwawanashindwa kwenda shule.
Suala la ambalo Diwani
wa Kata hiyo Nasir Salim Saum amesema yuko katika hatua mwisho ya ufuatiliaji
kwani mara nyingi amekua akiipigia kelele lakini changamoto ni ilikua pesa
hakuna hivyo ameahidiwa na halmashauri kuwa wataifanyia marekebisho barabara
hiyo.
Hatahivyo kwa upande wa
Mbunge Saumu Sakala amewaambia wananchi katika kata hiyo wawe kitu kimoja
katika kuijenga kata yao na pele wanaona ugumu wasiache kumshirikisha kwani
nyeye yupo kwaajili ya kuwatumukia wao.