Mafunzo hayo yameanza kutolewa
leo katika shule ya msingi funguni ambayo yalihudhuriwa na vikundi vitatu vya
wakina mama kikiwemo kikundi cha Amani Group,Jitihada na kikundi cha Muungano.
Ambapo katika mafunzo hayo
kinamama wenyewe wamekiri kutokuwa na uelewa wa kuviendeleza vikundi vyao na
kusemakuwa kutokana na mafunzo ambayo wameanza kuyapata leo yamewapa mwanganza
katika kuviendeleza vikundi vyao .
Halikadhalika mafunzo hayo
yalihudhuriwa na diwani wa pangani mashariki Mh AKIDA BORAMIMI ambapo amewataka
wakina mama kuzingatia mafunzo
wanayopata kutoka kwa muwezeshaji wa mafunzi hayo mwalimu JULIASI NGOMA .
Mafunzo ya kuwapa kinamama elimu
juu ya kuanzisha na kuviendeleza vikoba ama mifuko ya kijamii kwa
wakinamama wa
Pangani yameanza leo na yatatarajiwa kuisha tarehe 5/10/2016.