Katika kuhakikisha
wananchi wanapata maji safi na salama mbunge wa viti maalum Pangani SAUMU
SAKALA ametembelea kijiji cha mikinguni kitongoji cha kwang’ombe kuona jinsi
gani atawasaidia wanakijiji hao kupata maji safi na salama.
Wananchi hao
wamesemakuwa wamechimbiwa kisima na Islamic Help lakini maji ya kisima hicho ni
ya chumvi na hayafai kwa kunywa.
Hivyo inawabidi
kutembea umbali mrefu hadi katika vijiji vyenye maji safi kwa ajili ya kunywa
ikiwemo kijiji cha ushongo,mikinguni,na kasanga kwaajili ya kupata maji ya kunywa .
kwaupande wake Mwenyekiti
wa kitongoji RUKIA HAMZA amekiri kuwepo kwa shida ya maji katika kitongoji
chake lakini wameshindwa namna ya kufikisha maji kutoka mikinguni mjini hadi
kitongoji cha kwang’ombe.
Pia Mtendaji wa kjiji
cha mikinguni SALIMU MWAIPOPO amesema walishalifuatilia suala la ukosefu wa
maji ya kunywa katika kitongiji cha kwang’ombe katika idara ya maji pangani na
watu kutoka idara ya maji walishapima lakini umepita muda mrefu hadi sasa bado
hawajapewa mrejesho juu ya gharama ya kutoa maji kutoka mikinguni hadi kufika
katika kitongoji hicho.