Friday, September 23, 2016

MBUNGE SAUMU SAKALA ,JUMAA HAMIDU AWESO NA MKUU WA WILAYA PANGA BI ZAINABU WASUKUMA MBELE HARAMBEE YA KINAMAMA PANGANI


Mkuu wa wilaya ya pangani Bi Zainabu Abdallah akiwa pamoja na Mbunge wa viti maalum Saumu Sakala,na Mbunge wa jimbo la Pangani Jumaa Hamidu Aweso katika Harambee ya kuwachingia wakina mama wa kikundi cha AMANI GROUP cha Pangani Magharibi.

 Katika kuhakikisha kina mama wilaya ya pangani wanasonga mbele kimaendeleo leo kinamama wa kikundi cha AMANI GROUP cha Pangani Magharibi wameitisha kikao huku lengo la kikao hicho ni kufanya harambee ili kuwasaidia kinamama hao.


Na katika harambee hiyo iliyo hudhuruwa na Wabunge wa wilaya ya Pangani Mh Saumu Sakala na Mh Jumaa Hamidu Aweso huku Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi Zainabu Abdallah akiwa ndio mgeni mualikwa wa harambee hiyo.
Na huku Bi zainabu akiendesha harambee hiyo, Mbunge wa viti maalum Pangani Saumu Sakala ametoa  shilingi laki mbili,Mbunge Jumaa Hamidu Aweso ametoa laki tatu,mwenyekiti wa kata ya pangani magharibi laki tatu,katibu wa wafugaji wilaya laki mbili huku viongozi wengine wa vyama wakitoa fedha katika harambee hiyo.
Pia katika harambee hiyo Mbunge saumu sakala ameahidi kuwaletea wakinamama wa kikundi cha Amani Group Mwalimu wa kuwafundisha Ujasiria mali ili kipato cha wakinamama hao kuongezeka .

Na kwaupande wake Mbunge Jumaa Hamidu Aweso wakati akitoa neno katika harambee hiyo amewataka wakina mama hao kuandika barua ili kuweza kupa fedha zinazo tokana na mfuko wa jimbo.
kwaupande wake mkuu wa wilaya ya Pangani Bi Zainabu amewapongeza wakinamama hao kwaku thubutu kuanzisha kikundi chao kwa lengo la kuwakwamua wakina mama.
Lakini amewataka wakinamama hao kukisajili kikundi chao halmashauri ili hata wakati wa kutoka asilimia 5 ya halmashauri na wao wawezekupata fedha kwaajili ya maendeleo ya kikundi hicho.
Hatahivyo Bi Zainabu hakuwacha kuwashukuru wabunge kwakuacha mda wao na kukubali kuja katika harambee ya kikundi cha kinamama cha Amani Group cha Pangani Magaribi,na huku  akiwaomba kuwa pamoja katika kupeleka maendeleo ya Pangani mbele.
Hivyo  katika harambee hiyo ya kikundi cha kina mama cha Amani Group mkuu wa wilaya Bi Zainabu ametaja fedha zilizo patikana ni shililngi Milioni Moja Laki Saba na Elfu Arubaini Kwaajili ya kuwasaidia wakina mama hao.

Share:

Hon. Saumu Heri Sakala

Hon. Saumu Heri Sakala
Member of Parliment (MP)

Video

Recent Posts