Msingi wa ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Daluni uliogharimu shilingi Milioni 8 ambao kwa sasa umekwama zaidi ya miaka miwili |
Siku ya pili ya ziara
ya Mbunge Saumu Sakala katika wilaya mkinga ndani ya kata ya Daluni na Kata ya
Maramba ambapo lengo ni kusikliza changamoto mbalimbali zinazo wakumba wananchi
wa Wilaya ya Mkinga.
Akianzia katika kata ya
Daluni wakazi wa kata hiyo walifurahishwa na ziara ya Mbunge hiyo lakini
hawakuacha kumpa changamoto zinazowakabili katika kata yao.
Ambapo changamoto ya
Zahanati ndio ilikuwa kubwa ambayo inawafanya wakazi wa kata hiyo kutembea hadi
maramba mjini ilikupata huduma hiyo.
Ambapo katika
changamoto hiyo Mbunge alitakakujua mwenyekiti amelifuatiliaje suala hilo,hivyo
mwenyekiti alitoa tarifa ya kukwama kwa zahanati hiyo.
Mwenyekiti wa kitongoji
kata ya Daluni alisema kuwa zahanati hiyo ilipangwa kujengwa lakini mpaka sasa
ujenzi huo umeishia kwenye hatua ya msingi na kwa sasa ni miaka miwili imepita
kila wakilifuatila suala hilo majibu hakuna.
Pia mwenyekiti huyo
alimuambie mbunge kuwa ujenzi huo mpaka sasa umetumia shilingi milioni 8 suala
ambalo pia linawaacha wananchi mdomo wazi.
Hatahivyo Mbunge
alimtaka mwenyekiti kuatilia tena suala hilo kwani haiwezekani kiasi kikubwa
cha pesa kimetumika na zahanati ipo katika hatua ya msingi.
Vilevile katika hatua
nyingine wananchi hao wamelalamikia suala la kuto patikana na huduma ya
kupatikana kwa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto na kusema kuwa wanalazimika
kutembea hadi mkinga mjini.
Hivyo walimtaka Mbunge
kuwaombea huduma hiyo kusogozewa karibu kwani usumbufu wanaokutana nao ni
mkubwa ili kuweza kupata huduma hiyo.
Na kwa upande wake
Mbunge Saumu Sakala amewaahidi wakazi wa kata ya Daluni kuwa ataongea na RITA
ili kuweza kuwasogezea huduma hiyo karibu wakazi wa daluni hata kwa mwezi mara
,moja ilikuweza kuwaondolea wakazi hao usumbufu huo.
Pia changamoto ya
kukosekana kwa Tenki ya kuhifadhiwa maziwa hatua inayosababisha wafugaji wa
kata ya Daluni kutembea hadi maramba kupeleka maziwa yao.
Hivyo walimtaka Mbunge
awafuatilie suala la hilo katika uongozi wa Tanga Fresh ili waweze kupata Tenki
hiyo.
Halikadhalika katika
kata ya Maramba vitu vilivyo jitokeza ni kuuzwa kwa mbao ambazo zilikatwa kwa
lengo la kutengenezwa kwa mdawati ya shule ya Maramba.
Na changamoto inayo
wakwamisha ni kukosa fedha ya nauli ambayo itawafikisha hadi kwa mkurugenzi na
mkuu wa wilaya ilikulifuatilia suala la kuuzwa kwa mbao hizo.
Hivyo Mbunge
aliwawezesha Fedha ya nauli nakuwaambia kwa kilahatua watakayo fika wamjulishe
na pia mbunge amewaahidikuwapa ushirikiano juu ya kutatua suala hilo.
Ziara ya Mbunge Saumu
Sakala iliishia katika kata ya Maramba na kata ya Daluni ambapo ameahidi
kuyafuatilia yale yote ambao wamempa kwa lengo ya kuyatatua,