Wadau wa uvuvi wilayani pangani
wamesikitishwa na namna idara ya uvuvi wilaya humo inavyolishuhuliki suala la
uvuvi haramu.
Akiongea na
Saumusakalamp.blogspot.com mmoja wa wavuvi wilaya ya pangani Ndugu
KIMWERI ALI amesema
kuwa uvuvi wa kutumia baruti imekua ukitumika katika miamba ya bahari ya
pangani lakini idara ya uvuvi mpaka sasa haijachukua hatua yoyote kukabiliana
na suala hilo.
KIMWERI Ameogeza kuwa wamekua wakitoa
taarifa kwa idara hiyo juu ya matukia ya wavuvi wanatumia baruti katika uvuvi
lakini changamoto wanayokutana nayo ni baadhi ya watu idara ya uvuvi
wanamtandao na wavuvi haramu hivyo taarifa zao ni sawa na kutwanga maji
kwenye kinu.
Kwaupande wa mwenyekiti wa
pangani mashariki HAJI
NUNDU ambaye idadi kubwa ya wakazi wake ni wavuvi amesema kuwa
mara kwa mara serikali yake imekua ikitoa taarifa kwenye idara hiyo juu ya
wavuvi kutumia baruti pindi wanapokua baharini lakini majibu ya idara hiyo ni
kuwa BOTI haina mafuta ama BOTI haiko kwenye maji.
Hivyo kwa majibu mepesi ya idara
hiyo inaonyesha wazi kuwa nivigumu kupambana na uvuvi haramu wilayani pangani
kwakua idara husika imelala.
Kwaupande wake AMINA SULEIMAN ambaye alikaimu mkuu wa kitengo idara ya uvuvi wilaya ya pangani amesema kuwa
idara ya uvuvi inapambana na uvuvi haramu lakini changamoto ni idara hiyo
inapopata taarifa juu ya wavuvi kutumia baruti baharini mara nyingi boti inakua
haina mafuta na mlolongo wa kupata mafuta ni mrefu.
Hivyo ni vigumu kuwakamata wavuvi
wa baruti kwasababu mpaka unakamilisha
mlolongo wa kunapata mafuta wavuvi hao
wameshaondoka.
Pia boti ya inayotumiwa na idara
hiyo mara nyingi inakua haina mafuta ya hakiba kwaajili ya matumizi ya dharura
.