MWONGOZO
WA SPIKA ULIOOMBWA NA MHESHIMIWA ALLY
MOHAMED
KEISSY (MB) KUHUSU MALIPO YA POSHO
KWA
WABUNGE WANAOSUSIA MJADALA WA BUNGE
LA BAJETI
KWA KUTOKA UKUMBINI
WaheshimiwaWabunge, mnamotarehe 06 Juni, 2016 katikaKikao
cha Thelathini na Saba (37) cha Mkutano wa Tatu wa Bunge, Mheshimiwa Ally
Mohamed Keissy (Mb) aliomba Mwongozo wa Spika kuhusu Wabunge ambao wamekuwa wakisaini
kwa utaratibu mpya wa Kielektroniki (Biometric
Attendance Register)lakini baada ya hapo wanatoka Ukumbini bilakushiriki Mjadala
wa Bunge la Bajeti unaoendelea.
Hoja ya Mhe. Keissy (Mb) ilikuwa ni kutaka kujua
ni utaratibu gani utatumika kudhibiti vitendo hivi ili kuokoa fedha za Serikali
inayolipwa kama posho kwa Wabunge hao wanaosusia vikao vya Bunge la Bajeti.
Mhe.Keissy (Mb) alieleza kuwa kwa wiki Serikali inapoteza kiasi cha Shilingi Milioni
Arobaini na Mbili Mia Saba Sitini elfu (42,760,000/=) kwa kuwalipa posho Wabunge
hao wasiohudhuria vikao vya Bunge. Baada ya kuomba Mwongozo huo nilieleza kuwa nitalifuatilia
suala hili kuona namna nzuri ya kulishughulikia.
Vitendo
vya Waheshimiwa Wabunge kujisajili na
kasha kutoka ukumbuni vimekuwa vikiendelea kwa muda mrefu mpaka sasa na
jambo hilo
limekuwa likipingwa na kukemewa vikali nabaadhi ya Wabunge wanaobaki
ukumbini. Wabunge hao, kwa nyakati tofauti wamekuwa wakiomba
Mwongozo wa Kiti kuhusu kukubalika au kutokubalika kwa vitendo hivyo.
Tarehe
27 Aprili, 2016 Mhe. Hussein Mohamed
Bashe (Mb) ambaye alihoji endapo ni haki na sahihi kwa Wabunge hao
kupokea posho
wakati hawashiriki kutimiza wajibu wao wa Kikatiba na Kisheria.
Nikijibu Mwongozo huo nililieleza Bunge kuwa,
Bunge lina jukumu zito la kujadili Bajetiya nchi hivyo,kila Mbunge
anaowajibu wakushiriki
kikamilifu na kuchangia Bajeti jambo ambalo naamini ndicho wananchi
wanachokitazamia. Aidha nilieleza kuwa, inatakiwa uandaliwe utaratibu
mahsusi utakaowawezesha Waheshimiwa Wabunge kulipwa posho baada ya
kutekeleza majukumu
yao ipasavyo na sio kujisajili pekee.
Mnamo tarehe 30 Mei, 2016 Mhe.Dkt. Harisson
George Mwakyembe (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria nae aliomba Mwongozo kuhusu suala
hilo hilo baada ya kutoridhishwa na vitendo vya Wabunge kujisajili na kasha kutoka
nje ya ukumbi na kulipwa posho bila kufanya kazi. Mhe.Mwakyembe alinukuu Ibaraya 26(1) na (2)
za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ambayo inatoa nafasi kwa mtu
yeyote kuhoji kuhusu vitendo vinavyofanywa kinyume na Katiba. Aidha alisisitiza kwamba, kila mtu anapaswa kupata
ujira kulingana na kazi anazozifanya. Ibara ya 23(1) ya Katiba inaeleza ifuatavyo:-
“23(1)Kila
mtu, bila kuwapo ubaguzi wa aina yoyote, anayo haki ya kupata ujirau naolingana
na kazi yake na watu wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo
kulingana na kiasi na sifa za kazi wanazozifanya.”
Katika kujibu Mwongozo wa Mhe. Mwakyembe (Mb)niliendelea
kusisitiza kwamba Mbunge anatakiwa kulipwa mshahara au posho kutokana nakuhudhuria
na kushiriki mijadala Bungeni na kwa kuwa Wabunge ni wawakilishiwa wananchi katika
kusimamia Serikali, kutohudhuria Bungeni na kususia kutoa mchango wamawazo ni kushindwa
kutimiza wajibu wake wakibunge na kwamba si sahihi na halali kwa Mbunge kupokea
posho na mshahara bila kufanya kazi.
Vilevile,Mheshimiwa Ally Mohamed Keissy(Mb) kutokana
na kutoridhishwa na tabia hiyo ya Wabunge, aliwahi kuomba Mwongozo katika jambo
hilo katika Kikao cha 34 siku ya tarehe 01 Juni, 2016, . Alipoona
jambo hilo linaendelea na Wabunge wanaotoka ukumbini hawazingatii maelekezo ya Kiti,
mnamo tarehe 06 Juni, 2016 aliomba tena Mwongozo ambao ndio huu ninaoutolea maelezo.
Waheshimiwa Wabunge,nimetafakari kwa kina kuhusu vitendo
vya baadhiya Wabunge kutia saini, kuingia ukumbin na kasha kutoka nje ya ukumbi
nakuona kwamba endapo tabia hii itaachwa iendelee ninaamini itafika siku ambayo
Wabunge wote kwa ujumla wetu tutajisajili, kuingiau kumbini na kasha kutoka nje
jambo ambalo litasababisha shughuli za Bunge kutotekelezeka na hivyo kusababisha
kukiukwa kwa masharti ya Katiba yanayolipa Bunge hili majukumu ya kutekeleza.
Waheshimiwa Wabunge, Kanuni ya 5(1) ya Kanuni za Kudumuza
Bunge, Toleo la Januari, 2016 inaeleza kwamba Kiti kinapaswa kuzingatia pamoja na
mambo mengine, maamuzi yaawaliyaliyowahi kutole wa na Maspika wa Bunge. Katika suala
hili liloombewa Mwongozo, sawa na katika miongozo yaMhe. Bashe na Mhe.
Mwakyembe Bunge letu liliwahi kutoa Mwongozo kwenye suala la Wabunge kuingia ukumbini
na kasha kutoka njena hivyo kutoshiriki kwenye shughu lizilizopangwa.
Nimepitia maamuzi mbalimbali yaliyowahi kutolewa
na Bunge letu(Speaker’s Rulings)kuhusiana
na suala kama hili, hususani kuhusu vitendo vya Wabunge kutoka Ukumbini bila kutekeleza
shughuli rasmi za Bunge. Mnamo tarehe 8
Aprili, 2008, Wabunge wa Chama cha CUF walitoka Bungeni na kususia shughuli rasmi
zilizokuwa zimepangwa kutekelezwa kwa siku hiyo Bungeni. Kutokana na kitendo hicho
cha Wabunge wa CUF, Kiti kilitoa uamuzi ufuatao:-
“Kwa
sasa natamka tu kwamba Wabunge waliotoka nje ya Ukumbi kwa shughuli zisizokuwa rasmi
kwa maana ya Bunge hili basihawastahili kulipwa posho zinazohusika kwa sikuzote
ambazo watakuwa nje mpaka hapo tutakapotangaza utaratibu mwingine kwa sababu waliyokwenda
kuyafanya wala hayahusiani na shughuliza Bunge letu.”
Napenda kuwakumbusha Waheshimiwa Wabunge kwamba,
kwa mujibu wa Kanuni ya 146(1) ya Kanuni za Bunge, Wajibu wa kwanza wa kila Mbunge
ni kuhudhuria vikao vya Bunge na Kamati zake.
Jambo hili linapaswa kuzingatiwa na kila mmoja wetu.
Kitendo cha baadhi ya Wabunge kutoka nje mara baada
ya kujisajili na hivyo kutohudhuria vikao ni ukiukwaji wa Kanuni ya 146(1)
inayomtaka kila Mbunge kutekeleza majukumu yake kwa kuhudhuria vikao vya Bunge na
vikao vya Kamati.
Hivyo basi, kwa kuwa jambo hili halikubaliki na kwa
kuwa miongozo kadhaa imetolewa kuwasihi Waheshimiwa Wabunge wasitoke nje ya ukumbi
wa Bunge kwa shughuli zisizo rasmi, lakini vitendo hivyo vimekuwa vikiendelea na
hivyo kuleta tafsiri mbaya ya chombo hiki na kuathiri mwenendo mzima wa shughuli
za Bunge.
Kutokana na maelezo hayo pamoja na masharti ya Kanuni
ya 5(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge naagiza
kuwa, Wabunge wote wanao jisajili na kasha kutoka ukumbini kwa kususia kushiriki
mijadala ya Bunge hawastahili kulipwa posho kwa siku zote ambazo wamekuwa wakijisajili,
kuingi au kumbini na kasha kutoka ukumbini.
Huu ndio Mwongozo wangu.
Umetolewa leo 8 Juni, 2016.
Dkt. Tulia Ackson (Mb)
NAIBU
SPIKA