Wakiongea na mbunge wa viti maalumu kanda ya kaskazini
SAUMU SAKALA, wamesema wahamiaji hao wamesababisha uharibifu mkubwa
ikiwemo uharibifu wa mazingira na wizi wa mifugo.
Ambapo Mmoja wa wananchi hao swalehe swalo amewataja
wahamiaji hao ni pamoja na kabila la waduruma na wakamba, ambao hukata
miti, kuiba mifugo na kuuza kenya.
Hatahivyo Mh SAKALA amewatoa hofu wananchi wa kata SIGAYA juu suala hilo nakusema kuwa atalifikisha kwa waziri wa Ulinzi ili lipatiwe ufumbuzi.
Hayo yameibuka katika ziara yakuangalia maendeleo
mbalimbali sambamba na changamoto zinazowakabili wananchi wa wilaya ya
mkinga mkoani Tanga.