Wednesday, August 17, 2016
Friday, August 12, 2016
MBUNGE SAUMU SAKALA AMEANZA KUFUATILIA CHANGAMOTO ZA WANANCHI WA DALUNI -TANGA FRESH
Mbunge SAUMU SAKALA
amenza kufuatilia changamoto alilzokutana nazo katika ziara yake wilayani
mkinga katika Kata ya Daluni.
Leo mbunge Sakala
amekwenda katika kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh kufuatilia suala la
kupelekwa kwa mtungi wa maziwa kero ambayo imekua ikiwalazimu wakazi wa Daluni
kupeleka maziwa Maramba mjini.
Akiongea na mkuu wa
kitengo cha kusambaza Tenki hizo kwenye vituo ADAM NYEREMBE GAMBA amesema kuwa
amefurahishwa na hatua ya mbunge huyo kufuatilia suala hilo lakini kwa sasa
Tanga Fresh imekubwa na tatizo la kifedha hivyo kunaugumu wa kutekeleza ombi
hilo.
Adam amesema kuweka
mtungi ni gharama kubwa sana na pia mitungi hiyo haipatikani hapa nchini, kwani
mitungi hiyo inaagizwa kutoka nje ya nchi,hivyo nivigumu kuagiza mtungi mmoja.
Hivyo mkuu huyo
wakitengo amewataka wafugaji wa Daluni kupeleka maziwa yao Maramba kama hapo
awali walivyo kuwa wakifanya.
Pia kiwanda kipo katika
urekebishaji wa mfumo wa maji taka ambao urekebishwaji wake unagharimu pesa
nyingi sana ni Zaidi ya milioni 350.
Na wasipo rekebisha
mfumo huo kuna hatari ya kiwanda hicjo kufungiwa uzalishaji kwani walishapewa
notes na waziri wa mazingira kurekebisha mvumo wao wa maji taka
Pia kutokana
upatikanaji wa maziwa mengi katika wakati wa vuli hivyo kiwanda kimepanga
kufanya upanuzi wa kiwanda hicho na ujenzi huo utagharimu shilingi bilioni
12,hivyo utaona pesa itakayo tumika ni nyingi.
Hivyo Adam amewataka
wakazi wa Kata ya Daluni kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho kiwanda
cha Tanga fresh kipo katika hali mbaya ya kifedha na pindi mambo yakiwa mazuri
watapa Mtungu huo wa Maziwa.
MBUNGE SAUMU SAKALA AENDELEA NA ZIARA KATA YA DALUNI NA MARAMBA WILYANI MKINGA
Msingi wa ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Daluni uliogharimu shilingi Milioni 8 ambao kwa sasa umekwama zaidi ya miaka miwili |
Siku ya pili ya ziara
ya Mbunge Saumu Sakala katika wilaya mkinga ndani ya kata ya Daluni na Kata ya
Maramba ambapo lengo ni kusikliza changamoto mbalimbali zinazo wakumba wananchi
wa Wilaya ya Mkinga.
Akianzia katika kata ya
Daluni wakazi wa kata hiyo walifurahishwa na ziara ya Mbunge hiyo lakini
hawakuacha kumpa changamoto zinazowakabili katika kata yao.
Ambapo changamoto ya
Zahanati ndio ilikuwa kubwa ambayo inawafanya wakazi wa kata hiyo kutembea hadi
maramba mjini ilikupata huduma hiyo.
Ambapo katika
changamoto hiyo Mbunge alitakakujua mwenyekiti amelifuatiliaje suala hilo,hivyo
mwenyekiti alitoa tarifa ya kukwama kwa zahanati hiyo.
Mwenyekiti wa kitongoji
kata ya Daluni alisema kuwa zahanati hiyo ilipangwa kujengwa lakini mpaka sasa
ujenzi huo umeishia kwenye hatua ya msingi na kwa sasa ni miaka miwili imepita
kila wakilifuatila suala hilo majibu hakuna.
Pia mwenyekiti huyo
alimuambie mbunge kuwa ujenzi huo mpaka sasa umetumia shilingi milioni 8 suala
ambalo pia linawaacha wananchi mdomo wazi.
Hatahivyo Mbunge
alimtaka mwenyekiti kuatilia tena suala hilo kwani haiwezekani kiasi kikubwa
cha pesa kimetumika na zahanati ipo katika hatua ya msingi.
Vilevile katika hatua
nyingine wananchi hao wamelalamikia suala la kuto patikana na huduma ya
kupatikana kwa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto na kusema kuwa wanalazimika
kutembea hadi mkinga mjini.
Hivyo walimtaka Mbunge
kuwaombea huduma hiyo kusogozewa karibu kwani usumbufu wanaokutana nao ni
mkubwa ili kuweza kupata huduma hiyo.
Na kwa upande wake
Mbunge Saumu Sakala amewaahidi wakazi wa kata ya Daluni kuwa ataongea na RITA
ili kuweza kuwasogezea huduma hiyo karibu wakazi wa daluni hata kwa mwezi mara
,moja ilikuweza kuwaondolea wakazi hao usumbufu huo.
Pia changamoto ya
kukosekana kwa Tenki ya kuhifadhiwa maziwa hatua inayosababisha wafugaji wa
kata ya Daluni kutembea hadi maramba kupeleka maziwa yao.
Hivyo walimtaka Mbunge
awafuatilie suala la hilo katika uongozi wa Tanga Fresh ili waweze kupata Tenki
hiyo.
Halikadhalika katika
kata ya Maramba vitu vilivyo jitokeza ni kuuzwa kwa mbao ambazo zilikatwa kwa
lengo la kutengenezwa kwa mdawati ya shule ya Maramba.
Na changamoto inayo
wakwamisha ni kukosa fedha ya nauli ambayo itawafikisha hadi kwa mkurugenzi na
mkuu wa wilaya ilikulifuatilia suala la kuuzwa kwa mbao hizo.
Hivyo Mbunge
aliwawezesha Fedha ya nauli nakuwaambia kwa kilahatua watakayo fika wamjulishe
na pia mbunge amewaahidikuwapa ushirikiano juu ya kutatua suala hilo.
Ziara ya Mbunge Saumu
Sakala iliishia katika kata ya Maramba na kata ya Daluni ambapo ameahidi
kuyafuatilia yale yote ambao wamempa kwa lengo ya kuyatatua,
YALIO JIRI ZIARA YA MBUNGE SAUMU SAKALA KATA ZA SIGAYA,BOMA,MKINGA MJINI, NA KATA YA KWALE WILAYANI MKINGA
Mbunge Saumu Sakala akikagua Jengo la Shule iliyo Jengwa kupitia nguvu za wananchi katika kata ya Sigaya Wilayani Mkinga |
Mbunge Saumu Sakala
amendelea na ziara ya kata kwa kata wilaya kwa wilaya katikawilaya ya mkinga
kata ya sigaya.
Katika ziara hiyo
aliongozana na wenyeviti na diwani wa viti maalum kujua changamoto zinazo wakabili
wanakijiji wa kata ya sigaya iliyoko wilaya ya mkinga.
Mbunge amejionea
changamoto ya wahamiaji haramu kutoka kenya inayo wakabili wakazi wa kata hiyo,ambapo
wahamiaji hao wamekua wakiharibu mazingira kwa kukata miti na kwenda kuuza
kenya.
Wananchi hao pia
wamelalamikia suala la wizi wa mifugo unao fanywa na wahamiaji hao huku
wakisema wahamiaji ni kutoka kabila la waduruma na wakamba ambao baada ya kuiba
mifugo huenda kuuza kenya.
Kunyang’anywa kwa
vitambulisho vya ukazi kwa baadhi ya raia ambao ni WATANZANIA huku mamlaka
husika wilayani mkinga ikidai ni wahamiaji kutoka kenya.
Pia wananchi wa kata ya
sigaya wamelalamikia changamoto ya
kutokamilika kwa shule ya msingi iloiyojengwa kupitia nguvu za
wananchi,vyoo pamoja na kutokamilika kwa nyumba za wauguzi katika kata hiyo .
Suala ambalo Mbunge
Saumu Sakala amehuzunika sana hatua ya
shule iliyojengwa kupitia nguvu za wananchi na serikali kushindwa kuwasidia
wananchi hao kukamilisha shule hiyo.
Lakini kufuatia
changamoto hizo Mh Mbunge Saumu Sakala ameahidi kufuatilia matatizo hayo na
kuwaambia wana kata ya sigaya kuwa atakutana na Waziri wa mambo ya ndani juu ya
kupambana na suala la wahamiaji haramu kutoka kenya.
Pia mbunge saumu sakala
aliendelea na ziara yake katika kata tatu ambazi ni kata ya Boma Ndani ,Mkinga
Mjini,na kumalizia katika kata ya kwale ambapo alikutana na chamgamotom nyingi
ambazo kwanamna moja ama nyingine zinarudisha maendeleo ya wilayaya mkinga.
Miongoni mwa changamoto
hizo ni ubovu wa barabara katika kata ya Boma Ndani ambayo kwa wakati wa mvua
watoto wa shule huwawanashindwa kwenda shule.
Suala la ambalo Diwani
wa Kata hiyo Nasir Salim Saum amesema yuko katika hatua mwisho ya ufuatiliaji
kwani mara nyingi amekua akiipigia kelele lakini changamoto ni ilikua pesa
hakuna hivyo ameahidiwa na halmashauri kuwa wataifanyia marekebisho barabara
hiyo.
Hatahivyo kwa upande wa
Mbunge Saumu Sakala amewaambia wananchi katika kata hiyo wawe kitu kimoja
katika kuijenga kata yao na pele wanaona ugumu wasiache kumshirikisha kwani
nyeye yupo kwaajili ya kuwatumukia wao.
Thursday, August 11, 2016
KWAKAULI MOJA TUSEME NDOA ZA UTOTONI BASI
Shirika
lisilo la kiserikali la International Republican Institute (IRI) likishirikiana
na Mbunge wa vitimaalum Pangani Mh saumu sakala leo wamefanya kikao na
wakinamama wilayani pangani na lengo likiwa ni kuangalia usalama wa mtoto wa
kike kwa ujumla.

Kikao
hicho pia kimehusisha kuiangalia sharia ya ndoa ambayo kwa kipindi chote ilikua
ikimbana mtoto wakike ,ambayo sharia hiyo ilikua inaruhusu mtoto wa kike
kuolewa kuanzia miaka 15.
Mh
sakala ameongezea kuwa sharia hiyo ndio chanzo cha mimba za utotoni ambayo
madhra yake ni mwakubwa kwanza kwa mtoto wa kike na pili kwa mtoto anaye
mzaa,hivyo aliwataka wanawake kujadili kwa ilikupata njia thabiti ya kumlinda mtoto wa kike kwa maendeo ya
Taifa.
Pia
Muweezeshaji kutoka shirika la IRI
NORA PENDAELI aliwakaribisha wakinamama wa pangani kutoa mchango wao
kuhakikisha wazazi wanamlinda mtoto wa kike na kutokomeza janga la ndoa za
katika umri mdogo.
Akichangia
katika kikao hicho CHAUSIKU JUMA alisema ili kumlinda mtoto wakike ni lazima
kinamama kuwa kitu kimoja na kuona kuwa mtoto wa mwenzako ni kama mtoto wako
kwakufnya hivyo kutamfanya mtoto wa kike kuwa salama.
Kwani
maswahibu mengi yanayompata mtoto wa kike katika jamii ni kwakua wazazi hawana
umoja kila mzazi siku hizi humuangalia mtoto wake, hivyo kuwapa mwanya wanaume
kuwarubuni na kuwasababishia mimba watoto wakike.
CHAUSIKU
ameongezea kuwa katika suala la ndoa za utotoni zinaathari kubwa kwa watoto
wakike kwani mtoto wa kike mwili wake unakua hauja komaa kwahiyo madhara
anaweza kuyapata katika kujifungua,hivyo sio vizuri kwa kinamama kuwaoza watoto
wakike katikaumri mdogo.
Hata
hivyo mchangiaji wa pili AISHA MSOFE amesema kuwa licha ya madhara ya ndoa za
utotoni kuwa na athari kwa mtoto wakike lakini pia athari inakuja katika
familia kwani familia inabeba mzigo mkubwa baada ya mtoto wa kike kuachika
katika ndoa.
Pia
alisisitiza kuwa shariaya ndoa inayotakiwa kufanyiwa marekebisho ifike hatua
serikali iitekeleze matakwa ya sharia mpya itakayo pita kwa vitendo kwani mara nyingi imekua ikiishia kwenye
vitabu tu na kwaupande wa utekelezaji unakua mdogo.

Hivyo
utakuta mtoto wa kike kapatiwa mimba na mtoto wakiume lakini mamamzazi wa wa
mtoto wakike anashindwa kulipeleka suala mahakamani kisa alie sababisha
ujauzito ni mtoto wa jirani.
Hata
hivyo suala la elimu pia limeongele ambapo mchangiaji SOFIA MZINGA amesema kuwa
kufanyike kwa warsha na semina mara kwa mara kwa ajili ya kuwahamasisha wazazi
juu ya kuwalinda watoto wa kike ,kwakufanya hivyo itasaidia kupunguza matukio
ya mimba za utotoni.
Na
katika kuchingia suala la mimba za utotoni Mh SAUMU SAKALA amesema wazazi wananafasi
kubwa ya kuzuzi tatizo hilo kwani wanakaa sana na watoto hivyo wakiongea nao
vizuri na kuwaeleza madhara ya mimba katika umri mdogo watoto hawatashawishika.
Pia
Mh SAUMU SAKALA ameahidi kuyapeleka katika bunge la Jamuhuri ya Muungano Wa
Tanzania yale yote kinamama waliyo yaomba kwa niaba ya kumlinda mtoto wakike
kwa manufaa ya Taifa.
Hata
hivyo kikao hicho kimeadhimia kuanzisha jukwaa la kinamama kwa ajili ya
kujadili mipango mbalimbali lengo likiwa ni kuhakikisha mtoto wa kike anapiga
hatua mbele kwakupinga ndoa katika umri mdogo samaba na matumizi ya dawa za
kulevya.