Tuesday, August 9, 2016

HATIMAYE Russia na Uturuki zakubaliana kufufua uhusiano kati yao

Rais Vladimir Putin wa Russia na mwenzake Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki wamekubaliana kufufua uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kurejesha mawasiliano ya kibiashara na ujenzi wa mradi wa bomba la gesi asili.
Makubaliano hayo yalifikiwa jana kwenye mazungumzo kati ya marais hao wawili mjini St. Petersburg, Russia. Rais Putin amesema, Russia itaondoa vizuizi vya kuagiza bidhaa za Uturuki na makampuni ya Uturuki kufanya shughuli zao nchini Russia hatua kwa hatua. Aidha, pande hizo mbili zimekubaliana kutekeleza mradi wa ujenzi wa bomba la gesi asili na kituo cha uzalishaji wa umeme kwa nishati ya nyuklia nchini Uturuki.source http://swahili.cri.cn
Share:

Hon. Saumu Heri Sakala

Hon. Saumu Heri Sakala
Member of Parliment (MP)

Video

Recent Posts