Thursday, August 11, 2016

KWAKAULI MOJA TUSEME NDOA ZA UTOTONI BASI



Shirika lisilo la kiserikali la International Republican Institute (IRI) likishirikiana na Mbunge wa vitimaalum Pangani Mh saumu sakala leo wamefanya kikao na wakinamama wilayani pangani na lengo likiwa ni kuangalia usalama wa mtoto wa kike kwa ujumla.

Akiongea katika kiao hicho Mbunge Saumu Sakala amesema kuwa wameamu kukaa na kinamama wilaya ya pangani kutoka na hali ya ukatili wanao fanyiwa  watoto wakike katika jamii,ikiwemo ndoa za utotoni sambamba na mimba za utotoni.
Kikao hicho pia kimehusisha kuiangalia sharia ya ndoa ambayo kwa kipindi chote ilikua ikimbana mtoto wakike ,ambayo sharia hiyo ilikua inaruhusu mtoto wa kike kuolewa kuanzia miaka 15.
Mh sakala ameongezea kuwa sharia hiyo ndio chanzo cha mimba za utotoni ambayo madhra yake ni mwakubwa kwanza kwa mtoto wa kike na pili kwa mtoto anaye mzaa,hivyo aliwataka wanawake kujadili kwa ilikupata njia thabiti  ya kumlinda mtoto wa kike kwa maendeo ya Taifa.
Pia Muweezeshaji kutoka shirika la IRI NORA PENDAELI aliwakaribisha wakinamama wa pangani kutoa mchango wao kuhakikisha wazazi wanamlinda mtoto wa kike na kutokomeza janga la ndoa za katika umri mdogo.
Akichangia katika kikao hicho CHAUSIKU JUMA alisema ili kumlinda mtoto wakike ni lazima kinamama kuwa kitu kimoja na kuona kuwa mtoto wa mwenzako ni kama mtoto wako kwakufnya hivyo kutamfanya mtoto wa kike kuwa salama.
Kwani maswahibu mengi yanayompata mtoto wa kike katika jamii ni kwakua wazazi hawana umoja kila mzazi siku hizi humuangalia mtoto wake, hivyo kuwapa mwanya wanaume kuwarubuni na kuwasababishia mimba watoto wakike.
CHAUSIKU ameongezea kuwa katika suala la ndoa za utotoni zinaathari kubwa kwa watoto wakike kwani mtoto wa kike mwili wake unakua hauja komaa kwahiyo madhara anaweza kuyapata katika kujifungua,hivyo sio vizuri kwa kinamama kuwaoza watoto wakike katikaumri mdogo.
Hata hivyo mchangiaji wa pili AISHA MSOFE amesema kuwa licha ya madhara ya ndoa za utotoni kuwa na athari kwa mtoto wakike lakini pia athari inakuja katika familia kwani familia inabeba mzigo mkubwa baada ya mtoto wa kike kuachika katika ndoa.
Pia alisisitiza kuwa shariaya ndoa  inayotakiwa kufanyiwa marekebisho ifike hatua serikali iitekeleze matakwa ya sharia mpya itakayo pita kwa vitendo  kwani mara nyingi imekua ikiishia kwenye vitabu tu na kwaupande wa utekelezaji unakua mdogo.
ZAINABU YASINI mchangiaji katika kikao hicho amesema kuwa katika eneo la pangani matukio mengi ya yanayo wakumba wanawake yanashindwa kuchukuliwa hatua kutokana  na sababu ya kuweka udugu mbele.
Hivyo utakuta mtoto wa kike kapatiwa mimba na mtoto wakiume lakini mamamzazi wa wa mtoto wakike anashindwa kulipeleka suala mahakamani kisa alie sababisha ujauzito ni mtoto wa jirani.
Hata hivyo suala la elimu pia limeongele ambapo mchangiaji SOFIA MZINGA amesema kuwa kufanyike kwa warsha na semina mara kwa mara kwa ajili ya kuwahamasisha wazazi juu ya kuwalinda watoto wa kike ,kwakufanya hivyo itasaidia kupunguza matukio ya mimba za utotoni.
Na katika kuchingia suala la mimba za utotoni Mh SAUMU SAKALA amesema wazazi wananafasi kubwa ya kuzuzi tatizo hilo kwani wanakaa sana na watoto hivyo wakiongea nao vizuri na kuwaeleza madhara ya mimba katika umri mdogo watoto hawatashawishika.
Pia Mh SAUMU SAKALA ameahidi kuyapeleka katika bunge la Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania yale yote kinamama waliyo yaomba kwa niaba ya kumlinda mtoto wakike kwa manufaa ya Taifa.
Hata hivyo kikao hicho kimeadhimia kuanzisha jukwaa la kinamama kwa ajili ya kujadili mipango mbalimbali lengo likiwa ni kuhakikisha mtoto wa kike anapiga hatua mbele kwakupinga ndoa katika umri mdogo samaba na matumizi ya dawa za kulevya.
Share:

Hon. Saumu Heri Sakala

Hon. Saumu Heri Sakala
Member of Parliment (MP)

Video

Recent Posts