Mbunge SAUMU SAKALA
amenza kufuatilia changamoto alilzokutana nazo katika ziara yake wilayani
mkinga katika Kata ya Daluni.
Leo mbunge Sakala
amekwenda katika kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh kufuatilia suala la
kupelekwa kwa mtungi wa maziwa kero ambayo imekua ikiwalazimu wakazi wa Daluni
kupeleka maziwa Maramba mjini.
Akiongea na mkuu wa
kitengo cha kusambaza Tenki hizo kwenye vituo ADAM NYEREMBE GAMBA amesema kuwa
amefurahishwa na hatua ya mbunge huyo kufuatilia suala hilo lakini kwa sasa
Tanga Fresh imekubwa na tatizo la kifedha hivyo kunaugumu wa kutekeleza ombi
hilo.
Adam amesema kuweka
mtungi ni gharama kubwa sana na pia mitungi hiyo haipatikani hapa nchini, kwani
mitungi hiyo inaagizwa kutoka nje ya nchi,hivyo nivigumu kuagiza mtungi mmoja.
Hivyo mkuu huyo
wakitengo amewataka wafugaji wa Daluni kupeleka maziwa yao Maramba kama hapo
awali walivyo kuwa wakifanya.
Pia kiwanda kipo katika
urekebishaji wa mfumo wa maji taka ambao urekebishwaji wake unagharimu pesa
nyingi sana ni Zaidi ya milioni 350.
Na wasipo rekebisha
mfumo huo kuna hatari ya kiwanda hicjo kufungiwa uzalishaji kwani walishapewa
notes na waziri wa mazingira kurekebisha mvumo wao wa maji taka
Pia kutokana
upatikanaji wa maziwa mengi katika wakati wa vuli hivyo kiwanda kimepanga
kufanya upanuzi wa kiwanda hicho na ujenzi huo utagharimu shilingi bilioni
12,hivyo utaona pesa itakayo tumika ni nyingi.
Hivyo Adam amewataka
wakazi wa Kata ya Daluni kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho kiwanda
cha Tanga fresh kipo katika hali mbaya ya kifedha na pindi mambo yakiwa mazuri
watapa Mtungu huo wa Maziwa.