Bw Trump alikuwa amesema kwamba iwapo Bi Clinton atashinda basi atateua majaji wa Mahakama ya Juu ambao watafanikisha kuondolewa kwa haki ya raia kumiliki bunduki.
Alidokeza kwamba ni hatua ya raia pekee, ambayo inaweza kuzuia hilo lisifanyike.
Maafisa wa kampeni wa Clinton wameshutumu matamshi ya Trump na kusema ni hatari.
Lakini washauri wake wamesema alikuwa tu anawahimiza watu wanaoamini katika haki ya raia kumiliki silaha watumie kura zao kufanya uamuzi.source bbcswahili.com